Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.
Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper
Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo.
Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear na M
to the P ambaye walikuwa room moja wamekutwa wamezima baada
ya kuzidhisha madawa
ya kulevya...
Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki
leo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi
amefariki akiwa usingizini.
Akiongea na mwandishi wetu muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye
Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia
akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.
Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka na kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko
wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya
jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa
ameshafariki.
Jonathan amesema
hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa
kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo
nchini.
Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na
watu na makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia
kwenye mitandao ya kijamii.
Kilimanjaro Lager
Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji.
Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.
Ndovu Special Malt
R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many
Tanzanians.
Adam Nditi
Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta
#RIP #Mangwair #akaCowbama
Diva
Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t
believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?
R.I.P NGWAIR
0 comments:
Post a Comment