Kama ulikuwa haufahamu, Basi huyu ameumwa na buibui sehemu zake za siri huko Australia

post-feature-image

Mwanamume mmoja nchini Australia alilazimika kukimbia hospitalini upesi baada ya kuumwa na buibui mwenye sumu kali sehemu za siri.

Mwanamume huyo aliumwa na buibui huyo akitumia choo cha kusafirishwa eneo ambalo kunafanywa ujenzi mjini Sydney. Aliumwa na buibui aina ya redback katika uume wake. Msemaji wa hospitali ya St George Hospital alithibitisha kwamba mwanamume wa miaka 21 alifika hospitalini na kutibiwa.

Mtu anapoumwa na buibui hupata maumivu makali, kutokwa na jasho na pia kupata kichefuchefu.
Mwanamume huyo baadaye aliruhusiwa kuondoka hospitalini na matabibu wanasema maisha yake hayamo hatarini. Ingawa kumewahi kuripotiwa visa vya watu kufariki baada ya kuumwa na buibui aina ya redback, hakuna aliyefariki tangu kugunduliwa kwa dawa ya kumaliza sumu mwaka 1956.


Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment