1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh
Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40
Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu
shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa
inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya
Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali
Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini,
uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya
Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara
maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa
na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900).
Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century
Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye
thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia
40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian
inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa
za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye
thamani ya dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi
la makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya
dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na
thamani ya dola milioni 110 (shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la
makumpuni ya Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya
rejareja Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini
anayemwaga mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100 katika
mradi wa kustawisha mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi
milioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni
yake ya Khoja Shia Itnasheri Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo
ya maegesho ya magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi
bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi
sana wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa
sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio
na TV. Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya Morogoro, Mbeya na
Dar es Salaam. Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege
la Precision ambalo linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi
mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M
(Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo yenye
thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.
9. YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado
hakifahamiki lakini anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini
Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality
Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri
wake umeifaya timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili
katika orodha hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea
nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo tuliitoa
wiki iliyopita). Ni mmiliki wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania
Limited (METL) ambayo inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136 kwa mwaka
0 comments:
Post a Comment